Isaiah 32

Ufalme Wa Haki


1 aTazama, mfalme atatawala kwa uadilifu
na watawala watatawala kwa haki.

2 bKila mtu atakuwa kama kivuli cha kujificha kutokana na upepo
na kimbilio kutokana na dhoruba,
kama vijito vya maji jangwani
na kivuli cha mwamba mkubwa katika ardhi yenye kiu.


3 cNdipo macho ya wale wanaoona hayatafumbwa tena,
nayo masikio ya wale wanaosikia yatasikiliza.

4 dMoyo wa mtu mwenye hamaki utafahamu na kuelewa,
nao ulimi wenye kigugumizi utanena kwa ufasaha.

5 eMpumbavu hataitwa tena muungwana,
wala mtu mbaya kabisa kupewa heshima ya juu.

6 fKwa kuwa mpumbavu hunena upumbavu,
moyo wake hushughulika na uovu:
Hutenda mambo yasiyo ya kumcha Mungu,
na hueneza habari za makosa kuhusu Bwana;
yeye huwaacha wenye njaa bila kitu,
na wenye kiu huwanyima maji.

7 gTaratibu za mtu mbaya kabisa ni ovu,
hufanya mipango miovu
ili kumwangamiza maskini kwa uongo,
hata wakati ambapo hoja za mhitaji ni za haki.

8 hLakini mtu muungwana hufanya mipango ya kiungwana,
na kwa matendo ya kiungwana yeye hufanikiwa.

Wanawake Wa Yerusalemu


9 iEnyi wanawake wenye kuridhika sana,
amkeni na mnisikilize.
Enyi binti mnaojisikia kuwa salama,
sikieni lile ninalotaka kuwaambia!

10 jMuda zaidi kidogo ya mwaka mmoja,
ninyi mnaojisikia salama mtatetemeka,
mavuno ya zabibu yatakoma
na mavuno ya matunda hayatakuwepo.

11 kTetemekeni, enyi wanawake wenye kuridhika,
tetemekeni kwa hofu, enyi binti mnaojisikia salama!
Vueni nguo zenu,
vaeni nguo ya gunia viunoni mwenu.

12 lPigeni matiti yenu kwa ajili ya mashamba mazuri,
kwa ajili ya mizabibu iliyozaa vizuri

13 mna kwa ajili ya nchi ya watu wangu,
nchi ambayo miiba na michongoma imemea:
naam, ombolezeni kwa ajili ya nyumba zote za furaha
na kwa ajili ya mji huu wenye kufanya sherehe.

14 nNgome itaachwa,
mji wenye kelele nyingi utahamwa,
ngome ndani ya mji na mnara wa ulinzi vitakuwa ukiwa milele,
mahali pazuri pa punda na malisho ya makundi ya kondoo,

15 ompaka Roho amwagwe juu yetu kutoka juu,
nalo jangwa kuwa shamba lenye rutuba,
na shamba lenye rutuba kuwa kama msitu.

16 pHaki itakaa katika jangwa,
na uadilifu utakaa katika shamba lenye rutuba.

17 qMatunda ya haki yatakuwa amani,
matokeo ya haki yatakuwa utulivu
na matumaini milele.

18 rWatu wangu wataishi katika makao ya mahali pa amani,
katika nyumba zilizo salama,
katika mahali pa kupumzika pasipo na usumbufu.

19 sHata kama mvua ya mawe iangushe msitu
na mji ubomolewe kabisa,

20 ttazama jinsi utakavyobarikiwa,
ukipanda mbegu yako katika kila kijito,
na kuwaacha ng’ombe wako
na punda wajilishe kwa uhuru.
Copyright information for SwhKC